Pastor Ezekiel Odero aondolewa lawama na mahakama

Marion Bosire
1 Min Read

Mhubiri Ezekiel Odero ameondolewa lawama na mahakama ya Shanzu huko Mombasa baada ya upande wa mashtaka kukosa kumshtaki mhubiri huyo kwa makosa yoyote.

Mahakama hiyo pia ilifunga rasmi faili ya uchunguzi ya mhubiri huyo.

Serikali ilikuwa imemhusisha Odero na mhubiri tatanishi Paul Mackenzie ambaye amezuiliwa kutokana na vifo vya watu wengi ambao wanasemekana kuwa wafuasi wake kwenye msitu wa Shakahola.

Wawili hao waliaminika kuwa na uhusiano wa kibiashara hasa kupitia kituo cha runinga ambacho walikuwa wakitumia kueneza jumbe zao.

Awali kanisa lake la New Life Prayer Center liliondolewa kwenye sajili ya makanisa nchini na akaunti zake za benki zikafungwa lakini baadaye hayo yote yalibatilishwa.

Mahakama iliagiza pia kwamba mhubiri huyo arejeshewe shilingi milioni 1.5 ambazo alilipa kama dhamana ndipo akaachiliwa.

Share This Article