Papa Francis, kuonekana hadharani kwa mara ya kwanza Jumapili

Ni mara ya kwanza kwa Papa huyo kulazwa kwa kipindi kirefu zaidi hospitalini tangu achaguliwe miaka 12 iliyopita.

Dismas Otuke
1 Min Read

Papa Mtakatifu Francis anatarajiwa kuonekana hadharani kwa mara ya kwanza kesho,mwezi mmoja tangu alazwe hospitalini kutokana na  homa ya mapafu.

Papa aliye na umri wa miaka 88, alilazwa hospitalini Februari 14 mwaka huu ,akiwa tayari amelazwa kwa siku 37.

Ni mara ya kwanza kwa Papa huyo kulazwa kwa kipindi kirefu zaidi hospitalini tangu achaguliwe miaka 12 iliyopita.

Mfalme wa Uingereza Charles na Malkia Queen Camilla, wameratibiwa kumtembelea Papa mwezi ujao.

Website |  + posts
Share This Article