Panama yawatema wenyeji Marekani na kutinga fainali ya Gold Cup

Dismas Otuke
1 Min Read

Panama iliwatimua wenyeji Marekani kutoka kwa mashindano ya Gold Cup baada, ya kuwazabua mabao 5 -4, kupitia mikiki ya penati,kufuatia sare ya goli moja ndani ya dakika 90 katika nusi fainali iliyosakatwa Jumatano usiku mjini San Diego.

Iván Anderson aliwaweka Panama kifua mbele katika muda wa ziada kabla ya Jesus Ferreira kukomboa kwa Marekani na kulazimu mechi kuamuliwa kupitia penati.

Panama watamenyana na Mexico kwenye fainali baada ya Mexico kuwacharaza Jamaica mabao 3-0 katika semi fainali ya pili.

Share This Article
Leave a Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *