Serikali itatumia teknolojia kufanikisha uchumi wa saa 24 hapa nchini, amesema Waziri wa habari, mawasiliani na uchumi wa dijitali Eliud Owalo.
Waziri Owalo alisema taifa hili liko katika harakati za kuweka miundomsingi thabiti ya mfumo wa kidijitali na kuhakikisha kwamba kuna wataalam wa kutosha wa teknolojia ya habari ili kuhakikisha kwamba taifa hili linaweza kuzingatia na kutoa huduma zake kikamilifu kupitia mfumo wa kidijitali.
Akizungumza wakati wa uzinduzi wa maabara ya kidijitali Owalo aliyekuwa kwenye kaunti ya Nandi kwa hafla ya uzinduzi wa mahabara ya kidijitali katika taasisi ya kiufundi ya Tinderet, lililoko Taptengelei, eneo bnunge la Tinderet, Owalo alikariri kwamba hatua kubwa imepigwa katika utoaji wa huduma za serikali kupitia mfumo wa dijitali.
Uzinduzi wa mahabara hiyo utawezesha baadhi ya waliohitimu kutoka chuo hicho kupata ajioria katika baadhi ya mashirika ya kibinafsi yanayotoa huduma zao kwa mfumo wa kidijitali.
Viongozi waliohudhuria hafla hiyo walitoka wito kwa vijana kukumbatia ajira za mtandaoni, ikizingatiwa kuwa nafasi za ajira zinazidi kudidimia.