Operesheni ya Kursk: Vikosi vya Ukraine vyatishia kuteka eneo lingine la Urusi

Martin Mwanje
1 Min Read
Kifaru cha kijeshi cha Ukraine katika kilichoharibiwa wakati wa uvamizi wa Urusi

Wiki mbili baada ya uvamizi wa kikosi cha wanajeshi wa Ukraine katika eneo la Kursk, jeshi la Urusi bado halijaweza kuzuia kabisa mafanikio hayo.

Vikosi vya Ukraine sio tu kwamba vimepanua ukubwa wa eneo lililoteka, kuongeza wanajeshi wa akiba, lakini pia, muhimu zaidi, huenda linajiandaa kwa mashambulizi ya eneo jipya ndani ya Urusi, kwa ajili ya kukata mifumo ya usambazaji ya Urusi katika eneo la Glushkovsky lililopo katika jimbo la Kursk.

Moja ya hasara kwa Urusi kuhusiana na eneo ambalo vikosi vya Ukraine vilifanikiwa kuliteka katika mkoa wa Kursk ni kwamba, kwa asili, lilikuwa eneo dogo lililozungukwa pande tatu na ukanda unaodhibitiwa na Urusi.

Katika wiki mbili za mapigano, vikosi vya Ukraine havikuongeza mafanikio, lakini vilipanua wigo wa maeneo, na kushambulia maeneo ya kando katika jimbo hilo.

Share This Article