Operesheni ya Kiusalama yasababisha kupatikana kwa mifugo walioibwa

Tom Mathinji
1 Min Read
Operesheni ya kiusalama yabababisha kupatikana kwa mifugo walioibwa katika mpaka wa kenya na Ethiopia.

Huduma ya Taifa ya Polisi imetangaza kuwa operesheni iliyotekelezwa na asasi mbali mbali za usalama, imefanikisha kupatikana kwa mifugo walioibwa na majangali kutoka mpaka wa Kenya na Ethiopia katika eneo la Welegech Agosti 6, 2025.

Siku ya Jumapili kundi la maafisa wa usalama likiongozwa na Naibu Kamishna wa Kaunti wa Kokuro Evans Kimoni na Naibu Afisa Mkuu wa Polisi anayesimamia kituo cha polisi cha Kokuro kwa ushirikiano na Machifu na maafisa wa serikali, waliwapata ng’ombe wanane katika eneo la mpaka la Lowaat kati ya eneo la Kibish, Kenya na Dassanech Woreda nchini Ethiopia.

Huduma ya Taifa ya Polisi iliripoti kuwa upatikanaji wa mifugo hao ulifanikishwa kupitia ushirikiano na maafisa wa usalama kutoka Ethiopia, waliohakikisha mifugo hao wamrejeshwa salama nchini Kenya.

Maafisa kutoka pande zote walielezea kujitolea kuhakikisha usalama na amani zinadumishwa mpakani, wakielezea umuhimu wa kukabiliana na uhalifu mpakani.

Huduma ya Taifa ya Polisi iliwapongeza maafisa wote, viongozi wa eneo hilo na washirika waliohusika kwenye operesheni hiyo.

TAGGED:
Share This Article