OPEC: Muda wa kupunguza usambazaji mafuta kuongezwa

Tom Mathinji
1 Min Read

Nchi nane wanachama wa mataifa yanayozalisha mafuta, leo Alhamisi zimekubaliana kuongeza muda uliopo wa kupunguza usambazaji wa bidhaa za mafuta hadi mwishoni mwa mwezi Novemba 2024.

Nchi hizo zinazojumuisha Saudi Arabia, Urusi, Iraq, Muungano wa Milki za Kiarabu, Kuwait, Kazakhstan, Algeria na Oman, ziliahirisha mpango wa kuongeza usambazaji mafuta huku bei ya mafuta ghafi ikipungua.

kulingana na taarifa kutoka muungano wa mataifa hayo, Muda huo wa kupunguza usambazaji wa bidhaa za mafuta kwa mapipa milioni 2.2, utaongezwa kwa muda wa miezi miwili zaidi hadi mwezi Novemba mwaka 2024.

Juma lililopita, mataifa hayo yanayozalisha mafuta yakiongozwa na Urusi, yalitarajiwa kuongeza kiwango cha usambazaji mafuta.

Website |  + posts
TAGGED:
Share This Article