Seneta wa Busia Okiya Omtatah ni miongoni mwa waandamanaji waliokamatwa na polisi katikati ya jiji la Nairobi leo Jumatatu walipokuwa wakiandamana.
Waandamanaji hao walikuwa wakipinga ongezeko la visa vya utekaji nyara na kutoweka kwa watu kwa hali ya kutatanisha.
Omtatah akiwa na waandamanaji wengine yamkini walikataa kukamatwa na polisi na kujifunga kwa minyororo.
Waandamanaji hao wanapanga kufanya maandamano katika kaunti zote 47 nchini kupinga utekaji nyara.
Mkurugenzi wa Mashtaka ya Umma Mulele Ingonga ameagiza kufanywa kwa uchunguzi kuhusu utekaji nyara wa raia.
Uagizaji huo umeagizwa wakati miito ya kukomeshwa kwa utekaji nyara ikiongezeka, ya hivi punde ikitolewa na Jaji Mkuu Mstaafu David Maraga.