Omollo: Tutalinda uadilifu wa Mitihani ya Kitaifa

Tom Mathinji
1 Min Read
Katibu katiwa wizara ya Usalama wa Taifa Dkt. Raymond Omollo awasambazia wanafunzi mitihani.

Katibu katika wizara ya Usalama wa Taifa Dkt. Raymond Omollo, amesema serikali italinda uadilifu wa mitihani ya kitaifa, kupitia kushirikisha maafisa kutoka asasi mbali mbali wa kaunti ndogo zote.

Akizungumza leo Jumatano alipoongoza ufunguzi wa makaratasi ya mitihani katika afisi za kaunti ndogo ya Starehe, katibu huyo alisema usimamizi wa kiusalama wa mitihani ya kitaifa umeendeea bila hitilafu zozote tangu tathmini ya shule za msingi (KPSEA) na ile ya sekondari msingi (KJSEA) zilipoanza siku ya Jumatatu.

Hata hivyo, alikiri kuwepo kwa changamoto za kusafirisha mitihani katika baadhi ya maeneo hapa nchini, lakini alidokeza hatua mwafaka zimechukuliwa kufanikisha uwasilishaji wa mitihani kwa wakati.

Tathmini ya shule za msingi (KPSEA) zinakamilika rasmi leo Jumatano, huku wanafunzi milioni 1.29 waliofanya tathmini hiyo wakitarajiwa kujiunga na sekondari msingi.

Website |  + posts
Share This Article