Oduor asema miili iliyoopolewa Mukuru haina majeraha ya risasi

Marion Bosire
1 Min Read

Mwanapatholojia wa serikali Daktari Johansen Oduor jna alitoa ripoti yake baada ya kukagua miili ambayo ilitolewa kwenye timbo linalotumiwa kama jaa la taka mtaani Mukuru, kaunti ya Nairobi.

Kulingana na Oduor hakuna mwili ulikuwa na majeraha ya risasi na majeraha aliyoona ni ya kichwani kwenye mwili mmoja na kwamba mwili mwingine uliashiria kwamba marehemu aliuawa kwa kunyongwa.

Mkaguzi huyo wa maiti alielezea kwamba mifuko mingine iliyotolewa kwenye timbo hilo almaarufu Kware ilikuwa na miguu pekee ya binadamu.

Awali iliripotiwa kwamba miili 13 ilitolewa kwenye sehemu hiyo lakini baada ya ukaguzi, Oduor alisema kwamba miili ni tisa na nyingine ni sehemu tu za miili ya binadamu.

Alielezea kwamba miili hiyo iko katika viwango tofauti vya kuoza na imekuwa vigumu kwake kutambua kilichosababisha vifo vya ile iliyooza sana.

Miili hiyo ilipatikana kwa njia ya kutatanisha katika eneo la Kware baada ya mwanamke mmoja kudai kwamba dadake ambaye alipotea alimjia kwenye ndoto na kumwelekeza hadi uliko mwili wake.

Vijana wakazi wa eneo hilo walishirikiana na kuopoa miili hiyo kutoka kwenye timbo hilo ambalo lina maji na takataka nyingi na kuikabidhi maafisa wa polisi walioipeleka kwenye makafani ya City.

Share This Article
Leave a Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *