Odumbe ajumuishwa katika mpango wa Talanta Hela

Tom Mathinji
1 Min Read

Aliyekuwa nguli wa mchezo wa Kriketi hapa nchini Maurice Odumbe, ameteuliwa na wizara ya michezo kukuza mchezo huo hapa nchini.

Waziri wa michezo Ababu Namwaba alimpa fursa Odumbe kujiunga na mpango wa Talanta hela unaoendeshwa na wizara ya michezo, ili kutumia ujuzi wake wa kriketi kutambua na kukuza talanta za mchezo huo miongoni mwa chipukizi hapa nchini.

Akikubali fursa hiyo, Odumbe alisema atajizatiti kupeleka mchezo wa kriketi hapa nchini katika kiwango cha juu, na kuhakikisha inarejelea nafasi yake ya juu katika ngazi za kimataifa.

Hatua ya kumjumuisha Odumbe, ni sehemu ya mpango unaotekelezwa na waziri huyo, wa kuwajumuisha magwiji wa michezo katika ukuzaji wa talanta mbali mbali hapa nchini.

Miongoni mwa wanaspoti tajika ambao wamejumuishwa katika mpango huo ni pamoja na Allan Wanga, Wina Shilavula, Doreen Bwire na Wilfred Bungei.

Waziri wa michezo Ababu Namwamba alikuwa mwenyeji wa nguli  huyo wa mchezo wa kriketi, katika shughuli ya kumjulia hali mchezaji huyo.

Website |  + posts
Share This Article