OCS Taalam na wengine 5 kushtakiwa kwa mauaji ya Ojwang’

Tom Mathinji
1 Min Read
OCS Samson Talaam na washukiwa wengine 5 kufunguliwa mashtaka ya mauaji ya Albert Ojwang.

Washukiwa sita akiwemo Afisa anayesimamia Kituo cha Polisi cha Central Nairobi Samson Talaam, leo Jumanne wanatarajiwa kufunguliwa mashtaka ya mauaji ya mwanablogu na mwalimu Albert Ojwang.

Afisi ya kiongozi wa mashtaka ya umma (ODPP), tayari imependekeza washukiwa hao wafunguliwe mashtaka ya mauaji, ambao ni pamoja na   James Mukhwana, Peter Kimani, John Ngige Gitau, Gin Ammitou Abwao, na Brian Mwaniki Njue.

Siku ya Jumatatu walifikishwa kwenye mahakama ya Kibra, lakini hawakujibu mashtaka baada ya wawili kati yao kukosa mawakili wa kuwakilisha, hatua iliyomsababisha Justice Diana Kavenza kuahirisha kesi yao hadi Jumanne.

Ojwang  alitiwa nguvuni Juni 7,2025 katika kaunti ya Homa Bay baada ya kudaiwa kuchapisha habari za kupotosha dhidi ya Naibu Inspekta Mkuu wa Polisi Eliud Lagat.

Alizuiliwa kwa muda katika kituo cha polisi cha Mawego Police, kabla ya kusafirishwa hadi kituo cha polisi cha Central Nairobi, ambako alifariki mikononi mwa polisi.

Uchunguzi wa maiti ulibaini kuwa Ojwang alikuwa na majeraha kadhaa kichwani, kwenye shingo na sehemu zingine za mwili.

Website |  + posts
Share This Article