Obama: Raila alikuwa shujaa wa demokrasia

Tom Mathinji and BBC
2 Min Read

Rais mstaafu wa Marekani Barack Obama, ametaja aliyekuwa Waziri Mkuu wa Kenya Raila Odinga kama shujaa aliyepigania demokrasia sio tu nyumbani Kenya bali kote barani Afrika.

Katika ujumbe wake wa risala ya rambi rambi kwa wakenya, Obama alimkumbuka Odinga kama mtoto wa juhudi za kupigania Uhuru wan chi hasa ambaye baba yake alifungwa na serikali ya mbeberu kwa ajili ya kutaka kenya kuwa huru mnamo 1952.

‘Mara kwa mara nilipokutana naye, nilishuhudia akiweka taifa mbele ya haja zake za kibinafsi. Na kama viongozi wengine duniani alikuw atayari kufuata barabara ya kutaka maridhiano na upatanisho hata baada ya muda mgumu.’ Alisema Obama katika ujumbe wake.

Obama ambaye ana asili yake kutoka kaunti ya Siasa aliko zaliwa baba yake Hussein Obama, anamkumbuka Raila kwa jinsi alivyompa mapokezi mazuri alipofika nchini katika awamu ya kwanza ya uongozi wa Mwai Kibaki akiwa Seneta wa Jimbo la Illinois.

Raila aliandamana na Rais Obama kuelelea Kogelo kwa boma la babu yake alikoishi nyanya yake Sarah Obama alipokuwa akiishi.

Obama ambaye alikutana na kushirikiana na Odinga hasa alipokuwa Waziri Mkuu wa Kenya amesema pia, ‘maishani mwake, Raila alitoa mfano mkubwa sio tu kwa Wakenya na barani Afrika, bali duniani pia. Ninajua wengi watamkosa na kumbuka kwa dhati. Michelle nami tunatuma risala zetu za rambi rambi kw afamilia yake na raia wa Kenya,’ alimalizia Obama.

Website |  + posts
Share This Article