Takriban nyumba 1,000 huenda zikaathiriwa na mafuriko ambayo yatakayoletwa na mvua ya El Nino.
Mvua hiyo inatarajiwa kuanza baadaye mwezi ujao hadi Disemba.
Kulingana na Mamlaka ya Utabiri wa Hali ya Hewa nchini, nyumba hizo zilizo katika maeneo yapatayo 246 huenda zikaathiriwa na mafuriko.
Mamlaka hiyo imesema kuwa maeneo mengi humu nchini huenda yakashuhudia mvua za kadri na kiwango cha juu katika kipindi hicho na kuwataka wakazi wa maeneo hayo kuchukua tahadhari.
Maeneo hayo ni kama vile Uhuru Highway, Jogoo Road, Kangundo Road na Thika Road.
Mitaa inayotarajiwa kukumbwa na mafuriko ni Industrial Area, Pipeline, Kware na Imara Daima.
Pia katikati ya ya jiji la Nairobi inatarajiwa kuathiriwa na mafuriko.