Ruto kuzindua miradi ya kuwapiga jeki wafanyakazi wa sekta za kiufundi

Miradi hiyo inayojulikana kama Fundi Locater na ule wa NSSF Haba, itaendeshwa chini ya mpango wa uwezeshaji vijana wa NYOTA.

Dismas Otuke
1 Min Read

Rais William Ruto anatarajiwa kuzindua miradi ya kuwapiga jeki kiuchumi wafanyakazi wa sekta za Juakali na wale wa kazi za sulubu nchini Jumatatu ijayo.

Miradi hiyo inayojulikana kama Fundi Locater na ule wa NSSF Haba, itaendeshwa chini ya mpango wa uwezeshaji vijana wa NYOTA.

Katibu katika Wizara ya Leba Shadrack Mwadime, amesema miradi hiyo inalenga kuwawezesha vijana walio na ujuzi kama vile waashi,seremala,fundi wa umeme,wanajimu,makanika na wasusi.

Mpango wa Fundi Locater unalenga kuwaungnisha mafundi wa ujuzi kwa wateja wao huku ule wa NSSF Haba Haba ukiwajumuisha wafanyakazi wa sekta za kiufundi kuweka akiba ya uzeeni..

TAGGED:
Share This Article