Nyong’o: Nitaimarisha chama cha ODM

Tom Mathinji
1 Min Read
Gavana wa Kisumu Anyang' Nyong'o achaguliwa kiongozi wa muda wa chama cha ODM.

Kiongozi wa muda wa chama cha ODM Profesa Anyang’ Nyong’o, ametoa hakikisho la kutekeleza mikakati inayolenga kukiimarisha chama hicho, huku akichukua hatamu za uongozi kutoka kwa kiongozi wa muda mrefu wa chama hicho Raila Odinga.

Odinga ameondoka katika uongozi wa ODM, ili apate fursa ya kujiandaa kuwania wadhifa wa mwenyekiti wa Tume ya Muungano wa Afrika, AUC.

Kulingana na Nyong’o chama cha ODM kimepitia changamoto kadhaa na kwamba kitazidi kuwa thabiti huku akiwarai viongozi na wafuasi wa chama hicho kuunga mkono sera zake.

Gavana huyo wa kaunti ya Kisumu pamoja na maafisa wengine wa chama hicho wakati uo huo walipuuza madai kwamba chama cha ODM kimejiunga na serikali ya Kenya Kwanza wakisema chama chao kinajiandaa kuunda serikali baada ya Uchaguzi Mkuu ujao.

Share This Article