Nyachae ajiuzulu kutoka mahakama ya Afrika Mashariki

Dismas Otuke
1 Min Read

Charles Nyachae amejiuzulu wadhifa wa Jaji wa mahakama ya Afrika Mashariki, EACJ.

Kujiuzulu kwa Nyachae kulitangazwa rasmi wakati wa kikao cha kawaida cha 23 cha mahakama ya Afrika Mashariki katika kongamano na viongozi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, EAC.

EAC imeitaka Kenya kumteua mrithi wa Nyachae haraka iwezekanavyo.

Nyachae aliteuliwa mnamo mwaka 2018 na Rais Mstaafu Uhuru Kenya kuhudumu katika wadhifa wa jaji wa mahakama ya Afrika Mashariki, EACJ.

Share This Article