NRM kuelekea mahakamani kuhusu uchaguzi Kawempe Kaskazini

Mwaniaji wa NRM kwa jina Farida Nambi aliibuka wa pili kwa kura 8,593.

Marion Bosire
1 Min Read
Richard Todwong, Katibu mkuu wa NRM

Chama cha kisiasa kinachotawala nchini Uganda National Resistance Movement – NRM kinaripotiwa kutoridhika na matokeo ya uchaguzi mdogo wa ubunge katika eneo la Kawempe Kaskazini.

Inaripotiwa kwamba kamati kuu ya chama hicho iliandaa mkutano Ijumaa Machi 14, 2025 kujadili uchaguzi huo mdogo wa Machi 13, 2025 na matokeo yake.

Wanachama wa kamati hiyo wanaripotiwa pia kujadili kuhusu matukio ya uchaguzi huo kama vile madai ya udanganyifu na vurugu.

Chama hicho kinachoongozwa na Rais Yoweri Museveni hakikuridhika na matokeo ya uchaguzi huo mdogo ambapo Erias Luyimbazi Nalukoola wa chama cha upinzani cha NUP aliibuka mshindi.

Msimamizi mkuu wa uchaguzi katika eneo bunge la Kawempe Kaskazini Henru Makabayi alimtanaza Nalukoola mshindi baada ya kujipatia kura elfu 17, 764.

Chama cha NRM kimetangaza nia ya kuelekea mahakamani kupinga matokeo hayo ambapo mwaniaji wake kwa jina Farida Nambi alijipatia kura 8,593.

Katibu mkuu wa NRM Richard Todwong, alisoma taarifa ya baada ya mkutano wa kamati kuu ya chama.

Uchaguzi mdogo uliandaliwa katika eneo la Kawempe Kaskazini jijini Kampala kutafuta mbunge mpya kuchukua mahala pa Muhammad Ssegirinya wa chama cha NUP aliyeaga dunia mwezi Januari baada ya kuugua kwa muda mrefu.

Share This Article
Leave a Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *