Njugush ajibu madai ya JuaCali

Marion Bosire
1 Min Read

Mchekeshaji Njugush amesema hatishwi na wasiokubali kazi yake kama mchekeshaji. Aliyasema haya baada ya mwanamuziki JuaCali kutoa maoni kuhusu kazi yake ambapo alisema Njugush ana kipaji cha uigizaji na wala sio uchekeshaji.

Njugush ambaye jina lake halisi ni Timothy Kimani Ndegwa, alisema sanaa ina mitazamo tofauti na inagusa watu tofauti kwa njia tofauti.

“Video ya muziki ambayo unapenda labda mimi sitaipenda na hata sitaitizama. Ile ambayo ninapenda labda hautaipenda lakini haimaanishi hatufanyi kazi,” alisema Njugush.

Aliendelea kujipigia debe akisema kwamba ameandaa matamasha na kujaza kumbi mpaka nje ya nchi kama vile Amerika na Australia.

“Unajua ilivyo vigumu kujaza kumbi kule nje?” aliliza Njugush.

Alizungumzia kipindi cha kwanza ambacho aliigiza na ambacho wengi walidhania hakingeendela lakini kikapendeka zaidi. Kipindi hicho kinaangazia wafanyakazi wa nyumbani huko Kawangware.

Alisifia mitandao ya kijamii ambayo alisema kila mmoja anaweza kuchagua mwelekeo fulani wa kikazi na akaafikia ufanisi.

Alichochea wafuasi wake akiwataka wasubiri awamu ya tano ya onyesho lake almaarufu TTNT 5, ili waone kweli kama kazi yake sio nzuri.

Baadaye, mwanamuziki JuaCali aliwasiliana moja kwa moja na Njugush akamwomba msamaha na akasema hakuwa na nia ya kumdunisha.

Website |  + posts
Share This Article