Kiongozi wa muungano wa Azimio One Kenya Raila Odinga amesimama kidete akisema kuwa yuko tayari kuketi kwenye meza ya mazungumzo na Rais William Rito mbeke ya mpatanishi.
Kwenye mahojiano na shirika la habari la AFP, Raila amesema kuwa Rais William Ruto si mtu wa kuaminika maana hubadilisha msiamamo kila mara.
Hata hivyo, kiongozi huyo wa upinzani amekariri kuwa hana nia ya kugawana mamlaka na Ruto.
Raila amedai kuwa Ruto alidinda kukutana na Rais wa Tanzanaia Samia Suluhu aliyekuwa nchini kwa siku nia ya kuwapatanisha.
Juzi Jumanne, Rais Ruto alisema yuko radhi kukutana na Raila wakati wowote atakaopenda ili kuzungumzia masuala yanayomkwaza.
Raila amekuwa akiuongoza upinzani kushiriki maandamano katika kipindi cha wiki mbili zilizopita kulalamikia kupanda kwa gharama ya maisha na kushinikiza kutanguliwa kwa sheria ya fedha ya mwaka 2023.
Aidha upinzani unashinikiza mfumo wa uchaguzi kufanyiwa mabadiliko kabla ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2027, hatua inaosema itasaidia kuziba mianya ya udanganyifu katika chaguzi zijazo.
Hata ingawa Rais Ruto ameridhia kukutana na Raila, utawala wake umekariri kuwa hautashiriki ugavi wa mamlaka na upande wa upinzani kwa namna yoyote.