Timu ya taifaya Kenya ya soka ya wanawake Harambee Starlest imeratibiwa kuchuana Gambia, katika marudio ya raundi ya pili kufuzu kwa fainali za Kombe la mataifa ya Afrika (WAFCON) mwaka ujao nchono Morocco.
Starlets chini ya ukufunzi wa Beldine Odemba ilishinda mkumbo wa kwanza mabao 3-1, wiki jana na wanahitaji sare tu au hata kupoteza bao 1-0, dhidi ya wenyeji Gambia ili kufuzu kwa fainali hizo kwa mara ya pili.
Mchuano huo utachezewa nchini Senegal ambapo Kenya wanalenga kufuzu kwa kipute hicho kwa mara ya kwanza tangu mwaka 2016.
Pambano hilo litang’oa nanga saa moja usiku.