Ni kufa kupona kwa vipusa wa Kenya dhidi ya Cameroon leo

Mechi hiyo itang'oa nanga saa tatu usiku leo katika uwanja wa Olembe mjini Yaounde.

Dismas Otuke
1 Min Read

Timu ya Kenya kwa wasichana walio chini ya umri wa miaka 17,itamenyana na wenyeji Cameroon leo jini mjini Yaoundé, kwa mechi ya marudio raundi ya tatu, kufuzu kwa fainali za Kombe la Dunia.

Kenya ilishindwa bao moja kwa nunge katika duru ya kwanza uwanjani Nyayo Jumapili iliyopita .

Junior Starlets wanawania kufuzu kwa Kombe la Dunia kwa mara ya pili mtawalia baada ya kushiriki mwaka jana kwa mara ya kwanza katika Jamhuri ya Dominica.

Mechi hiyo itang’oa nanga saa tatu usiku leo katika uwanja wa Olembe mjini Yaounde.

Fainali za Kombe la Dunia zitaandaliwa mwishoni mwa mwaka huu nchini Morocco.

Website |  + posts
Share This Article