Waziri Mkuu wa Israel Prime Benjamin Netanyahu ameapa kuvunga runinga ya Al Jazeera nchini mwake akisema inaeneza ugaidi.
Tangazo la Netanyahu linaongoza tumbo joto kati ya Israel na Qatar ambayo inamiliki kituo hicho wakati ambapo serikali ya Qatar, imekuwa katika mstari wa mbele kuongoza maridhiano kati ya Israel na Wapalestina katika juhudi za kumaliza vita katika Ukanda wa Gaza.
Wanajeshi wa Israel walimuua mwanahabari mmoja wa Al Jazeera mjini Tel Aviv, wakati wa opereshini ya Gaza katika kile kilichotajwa baadaye na serikali ya Israel kuwa hayakuwa mauaji ya makusudi.