Neema apoteza katika raundi ya kwanza Olimpiki ya walemavu Paris

Dismas Otuke
1 Min Read

Mkenya Stency Neema ameshindwa katika raundi ya kwanza ya pigano la Taekwondo dhidi ya Salma Ali Abd Al Moneem Hassan kutoka Misri, katika uzani usiozidi kilo 52 katika michezo ya Olimpiki kwa walemavu inayoendela jijini Paris Ufaransa.

Neema amepoteza alama 3-12 kwenye pigano hilo lililoandaliwa katika ukumbi wa GrandPalais.

Mkenya mwingine Julieta Moipo atashuka ulingoni baadaye leo, katika pigano la chini ya uzani wa kilo 57 dhidi ya Micey Marija wa Serbia.

Website |  + posts
Share This Article