Ndege zisizo na rubani 114 za Ukraine zimedunguliwa – Wizara ya Ulinzi ya Urusi

Martin Mwanje
1 Min Read

Wizara ya Ulinzi ya Urusi inadai kuwa ndege zisizo na rubani 114 za Ukraine zimedunguliwa katika maeneo tofauti ya Urusi usiku kucha, na boti sita zinazojiendesha ziliharibiwa katika Bahari Nyeusi.

Hatahivyo wizara haiandiki chochote kuhusu ndege zisizo na rubani ambazo hazikudunguliwa na matokeo ya jumla ya uvamizi huo.

Kulingana na muhtasari wake mfupi, droni 70 “zilikamatwa na kuharibiwa” juu ya anga ya Crimea, 43 juu ya Wilaya ya Krasnodar na moja juu ya Mkoa wa Volgograd.

Kituo cha telegram cha Kirusi SHOT kinaripoti kwamba katika mji wa Krasnodar mtu mmoja alikufa kutokana na uvamizi huo baada ya kugongwa na droni au vifusi vyake

Usiku kucha, vituo vya habari vya Urusi na Ukraine vilichapisha video zilizochukuliwa na wakazi wa eneo hilo kuhusu milipuko katika eneo la Yeisk, ambapo kuna uwanja uwanja wa ndege wa kijeshi, Krasnodar na karibu na Krasnodar.

Share This Article
Leave a Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *