Nasreddine Nabi aondoka Yanga kwa makubaliano ya pande zote mbili

Francis Ngala
2 Min Read
Nasreddine Nabi

Klabu ya Young Africans (Yanga) nchini Tanzania, imethibitisha kuachana na Kocha Nasreddine Nabi baada ya kumalizika kwa mkataba wake mwishoni mwa msimu huu msimu.

Kupitia taarifa yake kwa umma iliyotundikwa katika mtandao wa Twitter klabu ya Yanga imesema kuwa ilikutana na kufanya mazungumzo ya kusaini mkataba mpya na Nabi lakini kocha huyo aliomba kuondoka ili akapate changamoto mpya.

Nabi anaondoka klabuni hapo siku tatu tu, baada ya kutwaa taji lake la sita ndani ya misimu miwili aliyoinoa klabu ya Yanga.

“Akiwa Kocha Mkuu wa Young Africans Sports Club, Nabi amefanikiwa kutwaa mataji mawili ya Ligi Kuu ya NBC, mataji mawili ya Kombe la Shirikisho la Azam, mataji mawili ya Ngao ya Jamii na kuifikisha timu yetu hatua ya fainali ya Kombe la Shirikisho la CAF.” imesema taarifa hiyo.

Nabi amendoka Yanga baada ya misimu miwili Tanzania: Photo – Unplayable

Mafanikio ya Nabi katika klabu ya Yanga yamemueka katika nafasi nzuri katika ulimwengu wa ukufunzi huku vilabu kadhaa barani Afrika na Mashariki ya Kati vikionyesha nia ya kumsajili kocha huyo.

Kaizer Chiefs ni mojawapo ya timu hizo na taarifa za kuaminika zinasema kuwa klabu hiyo imefanya mazungumzo na Nabi  Walakini, Nabi ameweka wazi njia zote kwa klabu yoyote inayomhitaji kwani ana ofa kadhaa mezani.

 

Share This Article
Follow:
I am Versatile Multimedia Journalist with years of experience in Digital platforms, Live TV and Radio. In another world am a News Anchor and Reporter.
Leave a Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *