Nandy avishwa pete nyingine na Billnass

Wawili hao waliandaa sherehe ya kuadhimisha miaka mitatu ya ndoa iliyohudhuriwa na wanafamilia na marafiki wa karibu.

Marion Bosire
1 Min Read
Billnass na mkewe Nandy

Wanandoa ambao ni wanamuziki tajika nchini Tanzania Nandy na Billnass wametimiza miaka mitatu kwenye ndoa na Jumanne jioni waliandaa sherehe ya kuadhimisha hilo.

Kwenye hafla hiyo iliyohudhuriwa na watu wa familia zao na marafiki wa karibu, Billnass alimvisha Nandy pete, yapata mwezi mmoja tangu alipotangaza kwamba amepoteza pete zake za ndoa katika mazingira ya kutatanisha.

Alipotangaza hilo, Nandy alitangaza zawadi ya shilingi milioni 10 pesa za Tanzania sawa na elfu 495 za Kenya kwa yeyote ambaye angmrejeshea pete hizo.

Kabla ya kumvisha Nandy pete hiyo, Billnass alisema kwamba mkewe amemvumilia sana katika kipindi cha miaka mitatu ambayo wamedumu kwenye ndoa.

Walipozungumza na wanahabari wanandoa hao walisema kwamba upendo umewasaidia sana kusuluhisha migogoro yao bila kuhitaji kwenda kwa wazazi au washauri wa ndoa.

Nandy alisema pia kwamba amepoteza marafiki wengi ambao mume wake hawataki kwenye maisha yao naye akalazimika kumtaka Billnass aachane na baadhi ya marafiki aliodai walikuwa wanachukua muda wake mwingi ambao anafaa kutumia kukaa na familia yake

Wasanii hao walifanya harusi Jumamosi Julai 16, 2022 na wana mtoto mmoja wa kike.

Website |  + posts
Share This Article