Nakhumicha: Huduma zinaendelea kutolewa hospitali za rufaa

Marion Bosire
1 Min Read

Waziri wa Afya Susan Nakhumicha amethibitisha kwamba huduma zinatolewa kama kawaida katika hospitali za rufaa nchini.

Aliyasema hayo wakati wa ziara yake katika taasisi mbalimbali za afya katika eneo la Nairobi wakati huu ambapo madaktari wanaendeleza mgomo.

Nakhumicha amesema hospitali za rufaa zinashuhudia ongezeko la wagonjwa wanaotafuta huduma na amwaehakikishia Wakenya kwamba watapata huduma bora za afya huku mazungumzo ya kutafuta kusitisha mgomo wa madaktari yakiendelea.

Aidha aliwahimiza wakenya kutafuta huduma za matibabu katika hospitali za rufaa kwa sasa.

Kuhusu bima mpya ya afya ya SHIF, Nakhumicha alisema kamati ya mpito kutoka NHIF hadi SHIF tayari imeweka mikakati ya kuhakikisha mpito usio na matatizo yoyote huku akihimiza Wakenya kujisajili kwenye mpango wa SHIF kwa wingi.

Aliongeza kuwa Wizara ya Fedha itatoa shilingi bilioni moja kwa NHIF ili iweze kukamilisha malipo yaliyosalia na akatoa hakikisho kwamba huduma hazitalemazwa wakati wa mpito.

Madaktari chini ya chama chao cha KMPDU wanaendeleza mgomo kulalamikia kutotekelezwa kwa matakwa yao na Wizara ya Afya, likiwemo hitaji lao la kuajiriwa kwa madaktari wanagenzi.

Share This Article