Nairobi United kuchuana na Gor Mahia fainali ya Mozzart bet Cup

Nairobi United waliopandishwa ngazi kushiriki ligi kuu ya FKF msimu ujao watapimana nguvu na Gor tarehe 14 mwezi huu kwenye fainali

Dismas Otuke
1 Min Read

Nairobi United itachuana na Gor Mahia katika fainali ya kombe la Mozzaert Bet, baada ya kuwabandua Mara Sugar, mwaoa 3-1 kupitia penati kwenye nusu fainali ya Jumapili.

Timu zote zilitoka sare ya bao moja ndani ya dakika 90, na kubidi matuta kupigwa ili kuwatenganisha mafahali hao wawili katika uwanja wa Dandora.

Nairobi United waliopandishwa ngazi kushiriki ligi kuu ya FKF, msimu ujao watapimana nguvu na Gor tarehe 14 mwezi huu ,kwenye fainali ,huku washindi wakiwahi tiketi ya kushiriki mashindano nya Kombe la Shirikisho msimu ujao.

Ni mara ya kwanza kwa Nairobi United, kufika fainali ya kombe la Mozzart Bet.

Gor walifuzu kwa fainali baada ya kuwatema nje Muranga Seal penati 5-4, kufuatia sare ya 2-2, katika semi fainali.

 

Share This Article