Idara ya utabiri wa hali ya hewa nchini (KMD) imetoa onyo la kuendelea kushuhudiwa kwa mvua kubwa katika kaunti ya Nairobi na viunga vyake.
Kwenye taarifa hiyo KMD imesema mvua za sasa zinatarajiwa kuendelea katika maeneo mengi hadi kufikia saa moja usiku Jumatatu, Machi 9 .
KMD imetaka wananchi kuwa waangalifu zaidi wakati wa mvua kutokana na mmonyonyo wa udongo.
Maeneo yanayotarajia kushuhudia mvua kubwa kesho Jumatatu katika kaunti ya Nairobi ni pamoja na Embakasi, Kibra, Makadara, Kamukunji, Roysambu, Westlands, Dagoretti, na Kasarani.
Aidha, kaunti jirani ya Kiambu inatarajia mvua kubwa katika maeneo ya Gatundu, Thika, Juja, Ruiru, Limuru, Kikuyu, Kabete na Githunguri, na pia kaunti ya Machakos katika maeneo ya Kathiani, Machakos Town, Matungulu na Yatta.