Naibu Rais Prof. Kithure Kindiki ameondoka hapa nchini kuelekea nchini Botswamna kuhudhuria sherehe ya kuapishwa kwa Rais Duma Boko aliyeibuka mshindi katika Uchaguzi Mkuu juma lililopita.
Kindiki anamwakilisha Rais William Ruto katika jukumu hilo, ambalo ndilo lake la kwanza tangu aapishwe kuwa naibu Rais.
Sherehe ya kumuapisha Rais Duma, itaandaliwa katika uwanja wa kitaifa wa Gaborone, leo Ijumaa.
Baadhi ya viongozi ambao wameandamana na Kindiki ni pamoja na Maseneta Fatuma Dullo (Isiolo) na Eddy Oketch (Migori), wabunge Owen Baya (Kilifi Kaskazini), Vincent Musyoka (Mwala), John Njuguna Kawanjiku (Kiambaa), Victor Koech (Chepalungu), na Elisha Odhiambo (Gem).