Maafisa wa tume ya maadili na vita dhidi ya ufisadi (EACC), wamewatia nguvuni maafisa wawili wa polisi kwa madai ya kuchukua hongo.
Kulingana na EACC, maafisa hao mmoja ambaye ni naibu wa OCS kaunti ya Kiambu George Chacha konstabo Elizabeth Mwongeli Muthoka, walikamatwa kwa kuitisha hongo ya shilingi 50,000 kutoka kwa mlalamishi ili gari lake liweze kuachiliwa kutoka kwa kituo hicho cha polisi licha ya agizo la Mahakama la kuachiliwa kwa gari hilo kutolewa.
“Wawili hao walikamatwa baada ya kupokea fedha hizo kutoka kwa mlalamishi katika kituo cha polisi cha Ikino,” ilisema taarifa ya EACC.
Kwa sasa wawili hao wanazuiliwa katika kituo cha polisi cha Milimani wakisubiri kufikishwa mahakamani.