Nadia Mukami achukua mapumziko kuangazia afya yake

Marion Bosire
1 Min Read

Mwanamuziki nyota wa Kenya Nadia Mukami ametangaza kwamba amechukua mapumziko ili aweze kuangazia afya yake.

Kupitia akaunti yake ya Instagram, mwimbaji huyo alielezea kwamba alizirai akiwa jukwaani wakati wa tamasha la Oktoba Fest, kutokana na matatizo ya ugonjwa wa pumu au ukipenda “asthma”.

“Nimekuwa mgonjwa kwa muda na baada ya wikendi hii nitachukua mapumziki hadi Novemba 15 ili kutunza afya yangu.” alielezea mwimbaji huyo.

Alishukuru wote ambao huwa anashirikiana nao kikazi kama vile wacheza densi wake, mpiga muziki na wasimamizi wengine kwa kumsaidia haraka alipopata matatizo.

Nadia alizindua albamu yake ya kwanza kabisa iitwayo “Queen of the East” ambayo amekuwa akiitangaza kupitia matamasha.

Share This Article