Mzee Yusuf Kaimu ambaye alikuwa maarufu nchini Tanzania kwa uigizaji na uchekeshaji alizikwa jana Oktoba 21, 2024.
Mwili wa mzee huyo aliyefahamika sana kama Pembe, ulizikwa kwenye makaburi ya Msikiti mweupe, eneo la Yombo Dovya Jijini Dar es salaam.
Aliaga dunia jioni ya Jumapili Oktoba 20, 2024, katika Hospitali ya Temeke Jijini Dar es salaam ambapo alikuwa amelazwa kwa matibabu.
Wasanii wenzake na wapenzi wa sanaa yake walihudhuria mazishi yake.
Marehemu ameacha Watoto 11 na amefariki akiwa na umri wa zaidi ya miaka 60.