Mwimbaji wa Marekani Fatman Scoop afariki akipiga tamasha

Dismas Otuke
1 Min Read

Msanii wa Marekani Fatman Scoop amefariki akiwa na umri wa miaka 53 baada ya kuanguka na kuzirai akiwatumbuiza mashabiki siku ya Ijumaa.

Kulingana na shirika la utangazi nchini Uingereza BBC,Scoop alikuwa katikati ya tamasha lake mjini Hamden nchini Marekani   alipozirai na kukimbizwa hospitalini .

Hata hivyo yamkini msanii huyo alifariki punde alipowasilishwa hospitalini na  Ambulensi.

Scoop ni msanii mashuhuri nchini Marekani akipiga mziki chapa ya Hip Hop tangu miaka ya 90 na alikuwa ameshinda tuzo kadhaa.

TAGGED:
Share This Article