Polisi wameanzisha uchunguzi kuhusu kifo cha kutatansiha ambapo mwili wa mwanamke mmoja wa umri wa miaka 24 ulipatikana Jumapili ukiwa umekatwakatwa viungo na kuwekwa ndani ya mfuko wa plastiki karibu na eneo la TRM barabara ya Thika.
Polisi wamesema hawajabaini chanzo cha mauaji hayo huku upasuaji ukitarajiwa kufanywa.
Mauaji hayo ni ya hivi punde baada ya mauaji ya Starlet Wahu Mwangi ambaye mwili wake ulipatikana kwenye chumba cha kupangisha mtaani South B.