Mwigizaji wa Nollywood Don Brymo ameaga dunia

Marion Bosire
1 Min Read

Mwigizaji wa muda mrefu nchini Nigeria au ukipenda Nollywood Don Brymo Uchegbu ameaga dunia.

Brymo wa miaka 56 anasemekana kukata roho akiwa usingizini usiku wa kuamkia leo.

Mayor Ofoegbu ambaye pia ni mwigizaji alidhibitisha kifo cha Brymo kupitia Facebook.

Anasema alipokea habari za kifo cha mwigizaji mwenzake kutoka kwa familia ya mwendazake asubuhi.

Anasema alichapisha maneno ya kuhimiza watu wapangie kesho lakini waishi Leo kwa sababu hawajahakikiahiwa kesho kwenye Whatsapp jana jioni na asubuhi akafahamishwa kwamba rafiki yake amekata roho.

Share This Article
Leave a Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *