Mwigizaji Dame Maggie Smith ameaga dunia

Tom Mathinji
1 Min Read
Dame Maggie Smith amefariki.

Mwigizaji Dame Maggie Smith, maarufu kwa filamu Harry Potter na Downton Abbey, amefariki akiwa na umri wa miaka 89, familia yake imesema.

Raia huyo wa Uingereza ameshinda mara mbili tuzo za Oscars katika taaluma yake mwaka 1970 na 1979 mtawalia.

Taarifa kutoka kwa watoto wake Toby Stephens na Chris Larkin ilisema,” Ni kwa huzuni kubwa tunatangaza kifo cha Dame Maggie Smith,”.

“Alifariki Ijumaa asubuhi akipokea matibabu hospitalini,” iliongeza taarifa hiyo.

Familia yake iliwashukuru maafisa wa matibabu ktika hospitali za Chelse na Westminster, kwa jinsi walivyomshughulikia mwigizaji huyo.

“Tungependa kuwashukuru wafanyakazi katika hospitali za Chelsea na Westminster kutokana na jinsi walivyomshughulikia Smith katika siku zake za mwisho,” ilisema taarifa hiyo.

Share This Article