Mwenyekiti wa Chama cha demokrasia na maendeleo (CHADEMA) Freeman Mbowe, amekamatwa na maafisa wa polisi katika eneo la Magomeni, Jijini Dar es Salaam leo Jumatatu.
Alikamatwa alipokuwa akiwahutubia wanahabari, huku chama hicho kikitisha maandamano ya kitaifa dhidi ya serikali.
Mnamo Septemba 11, 2024, Mbowe alitangaza kufanyika maandamano ya kulaani matukio ya watu kutekwa nyara na mauaji.
Hata hivyo, idara ya Polisi nchini humo kupitia msemaji wake, David Misime, imepiga marufuku maandamano hayo.
Kwa mujibu wa Mbowe, wameamua kuweka mkazo suala hilo, baada ya maombi ya mahitaji, ikiwemo kutaka kujiuzulu kwa Waziri wa Mambo ya Ndani, Hamad Masauni, viongozi waandamizi wa ulinzi na usalama kama sehemu ya uwajibikaji.
Amesema jambo lingine waliloliomba ni kurejeshewa kwa viongozi wa chama hicho, waliotekwa kwa nyakati tofauti wakiwa hai au hali ya umauti, akiwemo Deusdetith Soka, Dioniz Kipanya, Jacob Mlay na Mbwana Kombo.