Mwenyekiti wa bodi ya KUTRRH Olive Mugenda amejiuzulu

Tom Mathinji
1 Min Read
Olive Mugenda

Mwenyekiti wa bodi ya usimamizi wa hospitali ya mafunzo, utafiti na rufaa ya Kenyatta Olive Mugenda amejiuzulu. Hayo ni  kulingana na hatibu wa Ikulu Hussein Mohamed.

Kupitia kwa taarifa Jumanne usiku, Mohamed alisema Rais William Ruto amepokea na kukubali kujiuzulu kwa Mugenda, huku akimpongeza kwa mchango wake wa kupigiwa mfano, uliochochea ukuaji na maendeleo katika hospitali hiyo.

Wakati huo huo, Hussein alisema kufuatia kujiuzulu kwa Mugenda, bodi ya usimamizi ya hospitali hiyo imevunjwa mara moja na mchakato wa kubuni bodi mpya umeanza.

Afisa mkuu mtendaji wa hospitali hiyo Ahmed Dagane, ameagizwa na wizara ya afya kuenda kwa likizo mara moja, huku Dkt. Zainab Gura akiteuliwa afisa mkuu mtendaji wa hospitali hiyo.

Kulingana na arifa ya Hussein, Issac Kamau ambaye alikuwa ameteuliwa na bodi ya usimamizi ya hospitali hiyo kuwa kaimu afisa mkuu mtendaji, ameagizwa kusitisha jukumu hilo na kuripoti katika makao makuu ya wizara ya afya.

Mabadiliko hayo yamejiri baada ya wahudumu wa afya na wafanyakazi wa hospitali hiyo kugoma, wakilalamikia mazingira mabaya ya kazi, huku wakitoa wito kwa wizara ya afya kuingilia kati.

TAGGED:
Share This Article
Leave a Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *