Mwaura: Kubadilishiwa na kutuma maombi ya kitambulisho kipya ni bure hadi 2027

Martin Mwanje
1 Min Read
Isaac Mwaura - Msemaji wa serikali

Wakenya wanaotuma maombi ya kitambulisho kipya cha kitaifa kwa mara ya kwanza hawatatozwa ada yoyote hadi mwaka 2027. 

Aidha, wale wanaotaka kubadilisha vitambulisho vyao baada ya kupoteza vile vya awali hawatatozwa ada yoyote.

“Kubadilishiwa kitambulisho cha kitaifa kilichopotea na kutuma maombi kwa mara ya kwanza ni bure hadi mwaka 2027,” alisema msemaji wa serikali Isaac Mwaura wakati akiwahutubia wanahabari.

“Huduma Kenya imethibitisha kwamba kubadilishiwa kitambulisho cha kitaifa kilichopotea ni bure, hakuna anayepaswa kukutoza ada kufuatia agizo la Rais William Ruto la kuondoa ada kwa wale wanaotuma maombi kwa mara ya kwanza hadi mwaka 20227.”

Mwaura alisema hatua hiyo inalenga kuongeza idadi ya wanaotuma maombi ya vitambulisho vipya vya kitaifa hasa vijana na kuongeza idadi ya wanaojiandikisha kama wapiga kura kuelekea uchaguzi mkuu wa mwaka 2027.

 

Share This Article