Mwanazuoni Professa Martha Qorro, ambaye ni mmoja wa wahakiki wakuu wa lugha ya Kiswahili nchini Tanzania amefariki.
Prof. Qorro alifariki jana Jumatano.
Mwanazuoni huyo aliwahi kuhudumu katika wadhfa wa Mwenyekiti wa Baraza la Kiswahili Tanzania (BAKITA) na Mwenyekiti wa shirika la Haki Elimu.
Marehemu atakumbukwa daima kama mmoja wa wanaharakati waliopigania matumizi ya Kiswahili kama lugha ya kufundisha.