Mwanawe Muturi atoweka

Dismas Otuke
1 Min Read

Leslie Muturi mwanawe Mwanasheria Mkuu Justin Muturi angali hajulikani aliko baada ya kutekwa nyara Jumamosi usiku maeneo ya Lavington area.

Familia ya Muturi imethibitisha kutoweka kwa Leslie huku polisi wakikiri kutokuwa na fahamu kuhusu utekaji nyara huo .

Duru zaarifu kuwa Leslie aliye na umri wa miaka 40 alikuwa akitoka kwenye klabu cha Burudani karibu barabara ya Dennis Pritt, kabla ya kutekwa nyara muda mfupi baadaye.

Polisi wameanzisha uchunguzi huku chanzo cha utekaji nyara huo kikiwa hakijabainika.

Share This Article
Leave a Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *