Kukuza kikamilifu kilimo cha kijani hakuwezi kutimizwa bila ya uvumbuzi wa sayansi na teknolojia.
Katika miaka mingi iliyopita, wanasayansi na mafundi wengi wamekuwa wakishikilia kuendeleza mambo ya vijijini kwa njia ya kisayansi na kiteknolojia, jambo ambalo limeingiza msukumo mkubwa katika ujenzi wa vijijini.
Liao Hong, mwakilishi wa Bunge la 14 la Umma la China, ambaye pia ni mkurugenzi wa Kituo cha Utafiti wa Baiolojia cha Chuo Kikuu cha Kilimo na Misitu cha Fujian, na kamishna wa sayansi na teknolojia, ni mmoja kati yao.
Katika miaka ya 1990 ya karne iliyopita, Liao Hong alianza kujihusisha rasmi na utafiti wa baiolojia ya mizizi ya mimea. Anapenda somo hili, na ili kufanya nzuri, huwa anafanya majaribio kwenye maabara usiku kucha.
Matokeo ya kisayansi hayawezi kupatikana bila ya data halisi, hivyo mara nyingi aliwaongoza wanafunzi wake kufanya utafiti mashambani. Wakati wa majira ya joto, alikwenda shambani asubuhi mapema.
Hata hivyo anafurahia uzoefu kama huo, na uchovu wote huondolewa kutokana na kupatikana kwa matokeo ya kisayansi na kiteknolojia.
Katika majaribio hayo, Profesa Liao alipanda miche ya chai na mbegu za soya kwa pamoja, na kugundua kuwa, mizizi ya miche ya chai itakua kwa upande wa mizizi ya soya, na soya inatoa virutubisho vya asili kwa miche ya chai.
Kutokana na ugunduzi huo, Liao Hong alidhamiria kuleta teknolojia mpya kwa wakulima.
Alikwenda katika mashamba ya chai mkoani Fujian na kuona baadhi ya miche ya chai ilikuwa na majani membamba, na ni wazi kuwa ilikosa lishe bora ambayo ilisababishwa na matatizo kama vile ufanisi mdogo wa virutubisho na udongo mbaya.
Kutokana na hali hiyo, alipendekeza kujenga eneo la vielelezo la chai ya kiikolojia bila ya matumizi ya dawa ya kuua wadudu na mbolea ya kemikali.
Akaongoza timu ya ujumbe wa kisayansi na teknolojia kufanya majaribio ya bustani ya chai ya kiikolojia huko Wuyishan, kwa kupanda soya kati ya miche ya chai.
Mfumo huo wa kiikolojia umeingiza sayansi na teknolojia kwa upandaji wa chai, na kusaidia viwanda vya chai mkoani Fujian kupata maendeleo ya kijani yenye ubora wa juu.
Mwaka 2021, wakati rais Xi Jinping alipotembelea eneo hilo, alisifu kitendo cha “kupanda soya miongoni mwa miche ya chai” iliyobuniwa na timu ya Liao Hong, na kusema kuwa ustawishaji wa mambo ya vijijini unategemea uvumbuzi wa kisayansi na kiteknolojia.
Hii ilimtia moyo Liao Hong kuendelea na utafiti wake. Tangu mwaka 2015 hadi sasa, Liao Hong ameanzisha maeneo kadhaa ya chai yenye hali ya juu huko Wuyishan, Anxi na sehemu nyingine mkoani Fujian, na eneo la jumla linazidi hekta 667, kuwaandaa wataalamu wa kilimo zaidi ya 1000, na kuwafundisha wakulima zaidi ya 2,000.
Mwaka 2023 Liao Hong alichaguliwa kuwa mwakilishi wa Bunge la Umma la China.
Alisema matumaini yake ni kufanya matokeo ya utafiti wa kisayansi wenye hali ya juu kuwanufaisha zaidi wakulima, na yupo tayari kukusanya na kusikiliza sauti za wakulima, na kuwasilisha matakwa yao kwenye mkutano huo.