Mwanaharakati wa Iran Narges Mohammadi ashinda tuzo ya Nobel

Dismas Otuke
1 Min Read

Mwanaharakati wa haki za wanawake nchini Iran Nagres Mohammadi, ametangazwa mshindi wa tuzo ya amani ya Nobel mwaka 2023.

Bi Mohammed ametambuliwa kutokana na juhudi zake za kupigania haki za wanwake wanaokandamizwa nchini Iran,  na kupigania uhamasishaji wa haki za binadanu  na uhuru wa kila mtu.

Mohammadi amekamatwa na polisi mara kadhaa kwa kuongoza maandamano na hata kutumikia vifungo gerezani.

Narges Mohammadi,aliye na umri wa miaka  51, kwa sasa amefungiwa katika jela la  Evin mjini Tehran, akikabiliwa na kesi kadhaa ambazo zinahitajika hukumu ya kifungo cha miaka 12 kwa jumla.

Mohammadi  ndiye mwanamke wa 19 kutwaa tuzo hiyo ya amani.

Website |  + posts
Share This Article