Mwanahabari Rita Tinina apatikana amefariki nyumbani kwake

Dismas Otuke
1 Min Read

Mwanahabari mashuhuri wa KTN na NTV Rita Tinina amefariki .

Tinina ambaye hadi kifo chake alikuwa akifanya kazi katika runinga ya NTV amepatikana akiwa ameaga dunia nyumbani kwake mtaani Kileleshwa kaunti ya Nairobi.

Yamkini Tinina ambaye ni mama wa binti moja alikuwa aripoti kazini Jumapii na alipokosa kupatikana kwenye rununu yake ikabidi wenzake wafike kwake ndiposa wakapata mwili wake chumbani.

Tinina aliwateka watazamaji wengiu kutokana na jinsi alivyokuwa akiripoti taarifa za habari kwa nji ya kipekee na kwa weledi .

Polisi wameanzisha uchunguzi kuhusu chanzo cha kifo chake.

Mola ailaze roho yake mahala pema penye wema.

Share This Article