Mwalimu wa hisabati na kemia katika shule ya upili ya wavulana ya Nyamira, amejitoa uhai baada ya kupoteza shilingi 50,000 katika mchezo wa kamari.
Akithibitisha kisa hicho, naibu wa chifu wa mji wa Nyamira Johnson Manyara, alisema marehemu alijitia kitanzi chumbani mwake Jumatatano usiku.
Aliongeza kuwa, mke wa marehemu alikuwa amesafiri kuelekea mashambani baada ya kujifungua, na pia kuwajulia hali wazazi wa marehemu waliokuwa wagonjwa.
Mwalimu mkuu wa Nyamira, George Onkundi alieleza kuwa marehemu hakuonyesha ishara zozote za hali mbaya ila wakati mwengine aliomba walimu wenzake pesa na kukosa kuzirudisha.
Kulingana na mwalimu huyo mkuu, mwendazake alikuwa ameajiriwa na bodi ya shule na alikuwa amefunza kwa muda wa miaka minne.