Mvua za vuli kuanza katika maeneo kadhaa hapa nchini

Tom Mathinji
1 Min Read

Idara ya utabiri wa hali ya hewa imesema maeneo ya humu nchini ambayo yamechelewa kupokea mvua yataanza kupokea mvua wiki hii.

Kwenye utabiri wake wa siku 7 zijazo, idara hiyo imesema nyanda za juu mashariki ya Rif Valley, nyanda za chini kusini mwa nchi, eneo la pwani na eneo la kaskazini mashariki zinatarajiwa kushuhudia mvua nyakati za asubuhi na alasiri na rasha rasha za mvua nyakati za usiku katika sehemu chache.

Mkurugenzi wa idara hiyo Dkt. David Gikungu alisema nyanda za juu magharibi mwa Rift Valley, na eneo la ziwa victoria, zitaenedela kupokea mvua.

Hata hivyo amesema vipindi vya jua na ukavu vitaendelea kushuhudiwa baadaye wiki hii.

Viwango wastani vya joto vya zaidi ya nyuzijoto 30 vitashuhudiwa katika sehemu kadhaa za nchi ikiwa ni pamoja na kaskazini mashariki na kaskazini magharibi mwa nchi.

Viwango vya joto nyakati za usiku vitakuwa nuizijoto 10 katika eneo la Rift Valley.

Share This Article