Mvua inayonyesha katika maeneo mengi nchini inatarajiwa kuendelea mwezi Oktoba, kwa mujibu wa ripoti ya idara ya utabiri wa hali ya hewa iliyotangazwa leo Jumatatu jioni.
Maeneo yanayotabiriwa kupokea mvua nchini kati ya Oktoba 1 na 7 ni yale ya nyanda za juu, magharibi ya Bonde la Ufa, Ziwa Victoria na Nyanza.
Viwango vya joto vinatarajiwa kuwa kati ya nyuzi 10 na 37.
Hata hivyo, maeneo mengi nchini ikiwemo Kisii, Turkana, Samburu, Nyandarua, Laikipia, Nyeri, Kirinyaga, Murang’a, Kiambu, Meru, Embu, Tharaka Nithi na Nairobi yatapokea viwango vidogo vya mvua.
Maeneo ya nyanda za chini ya Machakos, Kitui, Makueni, Kajiado na Taita-Taveta yanatarajiwa kushuhudia jua.