Idara ya utabiri wa hali ya hewa, imetoa tahadhari kwamba maeneo ya kadhaa ya hapa nchini yatashuhudia kiwango kikubwa cha mvua kuanzia Alhamisi Novemba 14, 2024, kuanzia saa tisa alasiri na kuendelea hadi Ijumaa Novemba 15, saa tatu usiku.
Kulingana na utabiri huo, mvua itakuwa ya milimita 20 ndani ya saa 24, huku ikiongezeka hadi zaidi ya milimita 30 siku ya Ijumaa katika maeneo ya nyanda za chini ya Kusini Mashariki mwa nchi na maeneo ya Kati, Jiji la Nairobi likiwemo.
Hata hivyo, mvua hiyo inatarajiwa kupungua kuanzia Jumamosi Novemba 16, 2024.
Maeneo yanayotarajia kiwango hicho kikubwa cha mvua ni pamoja na Meru, Embu, Tharaka Nithi, Kirinyaga, Murang’a, Nyeri, Kiambu, Nyandarua, Laikipia, Isiolo, Nakuru, Kericho, Bomet, Narok, parts of Kajiado, Nairobi, Machakos, Kitui na Makueni.
Wakazi katika maeneo hayo wamtakiwa kujihadhari hasaa na uwezekano wa kutokea kwa mafuriko, hususan walio katika nyanda za chini.
Idara hiyo imeonya dhidi ya kuendesha gari au kutembea kwenye maji yanayoenda kwa kasi, na pia kujikinga mvua chini ya miti.